Warsha ya tathimini ya mapato ya biashara ya Kaboni na wadau kutoka Kijiji cha Masimba, Mvomero

Wadau mbalimbali wakiwemo Diwani wa Kata ya Pemba Mheshimiwa Coster Peter Reuben, viongozi wa Kijiji, Kamati ya Mazingira ya Kijiji na baadhi ya wanakijiji wa Masimba wamepata nafasi ya kushiriki warsha ya tathimini ya mapato ya biashara ya Kaboni iliyofanyika katika hoteli ya Ushetu, Turiani, Wilaya ya Mvomero tarehe 06/04/2025. Warsha hii ili lenga kutathimini uelewa wa wadau wa kijiji cha Masimba kuhusu matumizi ya mapato yatokanayo na biashara ya kaboni kama chanzo endelevu cha usimamizi shirikishi wa Msitu wa Masimba.

Warsha hii ya wadau wa kijiji cha Masimba imefanyika chini ya mradi wa kutathimini mapato yanayotoka na biashara ya Kaboni kama namna endelevu ya usimamizi shirikishi wa misitu unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo pamoja na Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni, NCMC.

Dkt. Kajenje Magessa Mhadhiri na Mtafiti wa SUA na Kiongozi Mkuu wa mradi amebainisha kuwa lengo la mradi ni kuangalia namna gani wanakijiji wanaoishi katika maeneo yanayozungukwa na Msitu wa Masimba wanaweza kuhifadhi msitu wao wenyewe kupitia mapato yanayotokana na biashara ya Kaboni kama chanzo endelevu cha fedha.