Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia watafiti wake kimezindua tathmini ya mapato ya Kaboni (Carbon) kama njia endelevu ya uwezeshaji kifedha katika uhifadhi na usimamizi wa misitu ya jamii Tanzania ambapo lengo la mradi huo nikusaidia jinsi gani mapato ya Hewa Ukaa yanaweza kusaidia kifedha katika kusimamia na kuhifadhi misitu ya jamii ambayo hairuhususiwi kwa uvunaji.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma Prof. Maulid Mwatawala akifungua washa hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma amesema kupitia Kaboni, SUA inakusudia kuendelea kusimamia misitu bila kuiathiri jambo litakalosaidia kupata kipato kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla.
Dkt. Kajenje Magessa Mhadhiri Mwandamizi wa SUA na Kiongozi Mkuu wa mradi amebainisha kuwa lengo la mradi ni kuangalia namna gani wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozungukwa na misitu (Katavi, Tanga, Morogoro, Manyara na Kilimanjaro) kuona ni namna gani wananchi wanaweza kuhifadhi misitu wenyewe bila kuiathiri na pia kwa namna nyingine kuwawezesha kupata mapato na kuepusha mabadiliko ya hali ya hewa
