Warsha ya tathmini ya mapato ya biashara ya kaboni ilifanyika tarehe 10/04/2025 katika hoteli ya Mvuni iliyopo Korogwe ikiwa ni sehemu ya mradi wa “Tathmini ya mapato yatokanayo na biashara ya Kaboni kama njia Endelevu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu nchini Tanzania”.
Wadau kutoka Vijiji vya Makangara na Gombero vya Korogwe, Tanga wakiwemo wanakijiji, Kamati ya Mazingira ya Kijiji, viongozi wa serikali za vijiji na Maafisa Misitu wa Wilaya ya Korogwe walipata nafasi ya kushiriki warsha hii. Mradi huu unashirikiana na jumuiya za wenyeji kutathmini uwezekano wa mapato ya biashara ya kaboni njia endelevu ya usimamizi shirikishi wa Misitu
Mradi huu unasisitiza kujenga uwezo kwa serikali za vijiji na washikadau ili kuelewa na kutumia kikamilifu fursa za masoko ya kaboni. Mpango huo unalenga kuimarisha uelewa na kutumia masoko ya kaboni ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kulinda viumbe hai na kupunguza umaskini katika Kijiji cha Makangara na Gombero, Korogwe, Tanga ikiwa ni kati ya maeneo ambayo mradi unatekelezwa.
Kwa kutathmini mapato ya biashara ya kaboni kama chanzo cha mapato cha Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) na kuimarisha uelewa wa washikadau kuhusu masoko ya hiari ya kaboni na bayoanuwai, mradi unalenga kudumisha USM na kuleta tija kwenye jamii inayozunguka misitu.



















